YANGA YAILIZA TENA BLACK LEOPARDS CCM KIRUMBA-MWANZA
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili
lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya
penati.
Golikipa wa timu ya Black
Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji
wa timu ya Yanga Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya
Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90 kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black
Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa
CCM-Kirumba jijini Mwanza.Picha na JICHIE BLOG-jijini Mwanza.
Mchezaji wa timu ya Yanga David Luhende akitaka
kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards, Moses Kwena, kwenye mchezo wao wa
marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya
leo.
Pichani ni Golikipa wa Black
Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa
kichwa na mchezaji wa Yanga, Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo
dakika ya saba.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za
kumtoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga
David Luhende akitaka kumtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards, Moses
Kwena, kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Baadhi ya mashabiki wa Mpira wakiwa wamepanga
mstari kwa ajili ya kununua tiketi na kujionea kandanda safi kabisa kati ya timu
ya Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya
pamoja.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia
mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya
Black Leopards ya Afrika Kusini, mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa
CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mtanange ukikaribia kuanza.
Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, mchezaji wa timu
ya Yanga, Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards, Jerry
alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha
pili.
Nginja nginja
tuu
Makocha wakipongezana mara baada ya mpira
kuisha.
Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya
Yanga.
Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia
uwanjani.
No comments:
Post a Comment