Wachezaji wa Atletico Madrid na Sevilla wakichuana usiku wa kuamkia leo katika nusu fainali ya Koimbe la Mfalme nchini Hispania |
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Atletico wa Vicente Calderon mjini Madrid na kuhudhuriwa na watazamaji 45,000 ilishuhudiwa magoli yote yakifungwa kwa penati.
Mikwaju miwili ya penati iliyotumbukizwa katika dakika ya 50 na 71 na Diego Costa na moja la dakika ya 56 la Alvaro Negredo wa Sevilla yaliweza kutoa matokeo ya mechi hiyo iliyokuwa kali.
Pia katika mechi hiyo ya jana ilishuhudiwa kadi nyekundu tatu zikitolewa kwa wachezaji watatu, mmoja wa Madrid na wawili wa Sevilla baada ya kuonyeshwa kadi za njano awali.
Sasa Atletico itasubiri mpaka baada ya pambano lao la marudiano na wapinzani wao watakaokuwa nyumbani Februari 27 kujua hatma yao ya kucheza fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya wapinzani wa jadi Barcelona na Real Madrid zilizotoshana nguvu juzi kwa kufungana bao 1-1 kwa ajili ya fainali ya michuano hiyo.
Fainali hizo zinatarajiwa kuchezwa
wenyeji walisubiri hadi kipindi cha pili kujihakikishia ushindi huo.
No comments:
Post a Comment