Nahodha wa Cameroon, Samuel Et'oo |
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa
Miguu Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji
21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na nahodha Samuel Et’oo
Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi wa msafara wa
timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni
Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara
wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT,
John Ndeh.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema mbali ya Et’oo,
wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou
Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam,
Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean
Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre
Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine ni Andre
Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu),
Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk.
Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia wapo Tchonkontey
Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team
Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja
Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem
(Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).
Wakati huo huo, kikosi
cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini
kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.
No comments:
Post a Comment