Aliyekuwa kocha wa Yanga, Tom Saintfiet aliposhuhudia kipigo cha Mtibwa kabla ya kutimuliwa. |
Wachezaji wa Yanga na Mtibwa walipokuwa wajiandaa kuumana katika duru la kwanza ambapo Yanga ililala mabao 3-0 |
Yanga ilinyukwa mabao 3-0 na Mtibwa katika pambano lao la duru la kwanza, hivyo itashuka dimbani kesho kwa nia ya kuendeleza wimbi la ushindi sambamba na kulipa kisasi cha mabao hayo.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, waliokuwa ughaibuni nchini Uturuki kujiandaa na duru hilo la pili, imetamba kuwa kesho ni zamu yao ya kucheka mbele ya Mtibwa.
Mechi nyingine za kesho ni katio ya Polisi Moro iliyopo mkiani mwa msimamo itakayovaana na African Lyon, mjini Morogoro na Mgambo JKT ya Tanga yenyewe itakuwa dimba la Mkwakwani kuvaana na Ruvu Shooting.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba wenyewe watashuka dimbani Jumapili kwa kuvaana na JKT Ruvu, huku Coastal Union ya Tanga itaialika Prisons ya Mbeya uwanja wa Mkwakwani.
Mpaka sasa Yanga ndio wanaoongoza msimamo wakiwa na piointi 32 wakifuatiwa na Azam kisha Simba zilizopo nafasi ya pili na tatu.
No comments:
Post a Comment