STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 8, 2013

Abdi Kassim 'Babi' aendeleza rekodi zake kimataifa

Abdi Kassim 'Babi'

MCHEZAJI Abdi Kassim 'Babi' ameweka rekodi nyingine katika historia ya soka ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Azam kufunga bao kwenye mechi ya kimataifa tangu timu hiyo iundwe.
Bao alilofunga dakika ya 14 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Al Nasri ya Juba nchini Sudan ya Kusini limemfanya aingie kwenye rekodi hiyo.
Mechi hiyo ilichezwa uwanja wa Taifa, Azam ilitoka na ushindi wa bao 3-1, kabla ya kwenda kushinda tena ugenini bao 5-0, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya bao 8-1.
Kwenye uwanja wa Taifa, mbali na Babi, mabao mengine mawili ya Azam yalifungwa na Kipre Tchetche.
Azam  ilianzishwa mwaka 2007 na kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2008, kabla ya kufanikiwa kucheza michuano ya kimataifa mwaka huu na kuziacha .
Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, anayefahamika pia kama 'Barack wa Unguja' amejiongezea rekodi hiyo baada ya ile ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza katika uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam mara tu ulipofunguliwa.
Rekodi hiyo aliiweka mwaka 2007 kwenye mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Uganda Cranes iliyokuwa ya ufunguzi rasmi ya uwanja huo pamoja na kujiandaa na mechi dhidi ya Msumbuji iliyokuwa ya kusaka kwenda Ghana ilikochezwa fainali ya Afrika mwaka 2010.
Bao hilo alilifungwa dakika ya 54 kwa shuti kali umbali wa mita 18 baada ya gonga vizuri kti ya Said Maulid na Haruna Moshi 'Boban'.

No comments:

Post a Comment