Mlezi wa timu ya Golden Bush Veterani, Onesmo Waziri 'Ticotico' akihojiwa na wanahabari |
Pambano hilo maalum kwa Golden Bush ikijiandaa kuwavaa wapinzani wao wa jadi, Wahenga Fc wakati wa sikukuu ya Pasaka, lilioshuhudiwa Golden Bush wakianza kupata bao kupitia 'Pro' wao kutoka Kongo, Sadick Mihambo kabla ya Baker Rangers iliyokuwa na nyota kama Mussa Hassani Mgosi, Abuu Ramadhani 'Amokachi', Kamba Luffo na mkongwe Abdallah Kinyunyu ilisawazisha bao hilo.
Mfungaji wa bao hilo la kusawazisha lililofanya hadi mapumziko timu zote kutoka nguvu sawa uwanjani, lilipachikwa wavuni na Kinyunyu.
Kipinsi cha pili timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu, japo hazikuweza kuongeza bao lolote na kufanya hadi pambano lilipomalizika ziwe sare ya bao 1-1.
Mlezi na Msemaji wa Golden Bush aliyeipenyezea Blog hii matokeo ya mechi hiyo, alisema wamefarijika kupata sare hiyo, japo walipania kuibuka na ushindi, huku wakidai pambano hilo limekuwa kipimo tosha la kujiandaa na mechi yao dhidi ya Wahenga watakaomenyana nao wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Golden Bush na Wahenga zimeshakutana mara tatu mpaka sasa na kila moja kuibuka na ushindi wa mechi moja na pambano jingine kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1, na msemaji huyo wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' amedai mechi yao ijayo ni lazima watainyamazisha Wahenga ili kuisherehekea vema sikukuu ya Pasaka.
No comments:
Post a Comment