STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 10, 2013

Ushindi Simba yafufua matumaini, wazima 'uasi' Msimbazi


Haruna Chanongo akijiandaa kufumua shuti katika lango la Coastal Union

USHINDI wa mabao 2-1 iliyopata Simba jioni ya leo licha ya kufufua matumaini yao ya kutetea taji lao ambalo linaoonekana kunyemelewa na Yanga, lakini pia imefanikiwa kuzima hasira za mashabiki wake ambao wamekuwa wakitoa shinikizo la viongozi wa klabu hiyo kuachia ngazi kwa timu kufanya vibaya.
Aidha kufanikiwa kufunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza kwa Simba kumekuwa kama rekodi kwao kwani karibu mechi zote imekuwa ama ikienda mapumziko wakiongoza kwa bao moja kupata ushindi wake katika kipindi cha pili tofauti na ilivyokuwa leo mbele ya Wagosi wa Kaya.
Mashabiki wa Simba wamekuwa na hasira na timu yao kutokana na kuwanyima raha tangu mwishoni mwa duru la kwanza mwishoni mwa mwaka jana kwa kupoteza mechi au kuambulia sare kiasi kwamba imesababisha baadhi ya viongozi wake kuamua kiuachia ngazi huku mashabiki hao wakiwa na hamu ya Simba ingeteleza leo ili wawe na sababu ya kuuong'oa uongozi mzima chini ya Ismail Aden Rage.
Hata hivyo mabao mawili ya Mrisho Ngassa na Haruna Chanongo yalitosha kuzima 'uasi' Msimbazi kwa kuongeza hazina ya pointi katika mbio zao za kutetea taji la ligi kuu.
Hata hivyo Simba italazimika kupata ushindi katika mechi zake saba zilizosalia huku wakiiombea Yanga na hata Azam ziteleze katika michezo yao ili kuweza kulitetea taji lake, vinginevyo wanaweza kujikuta wakiikosa hata nafasi ya pili.
Yanga yenye pointgi 45, inahitaji pointi 14 tu katika mechi zake saba zilizosalia kuweza kujihakikishia ubingwa na 12 tu kufikisha pointi 57 ambazo zitaivua Simba taji kwani mabingwa hao watetezi uwezo wa kwa sasa ni kufikisha poingti 55 tu.
Hata hivyo kwa vile soka halitabiriki na Simba na Yanga zenyewe zinatarajiwa kukutana katika mechi ya marudiano itakayofungia msimu Mei mwaka huu, yanaweza kutokea maajabu kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita ambapo Yanga iliwazidi kete Simba dakika za mwishoni na kuwapoka taji kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa baada ya muda mrefu kuachwa nyuma na watani zao hao pamoja na Azam walioambulia nafasi ya tatu msimu wa 2010-2011.



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































No comments:

Post a Comment