MZIMBA AGONGWA NA BODABODA, RAIS KIKWETE AMTEMBELEA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba,
mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye
amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha
kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini
Dar es salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa
kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana hali yake
ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole kwa maumivu
aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment