TUZO ZA MUZIKI ZA KILI 2013 ZAZINDULIWA
TUZO za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
George Kavishe, Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”
Alisema Kilimanjaro Premium Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka wanamuziki wetu wajisikie wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya vile vile tunataka Watanzania waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio hili litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia tuna furaha kutangaza kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment