STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 21, 2013

Banka ataka TFF ifuatilie nyota waliopo nje ya nchi

Mohmmed Banka (kulia)
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Kenya, Mohammed Banka amesema ipo haja ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatilia nyendo za wachezaji wa kitanzania wanaocheza nje ya nchi ili waweze kupata fursa ya kulitumikia taifa lao katika mechi za kimataifa.
Banka anayeichezea timu ya Ligi Kuu ya Kenya, Bandari ya Mombasa, alisema nje ya nchi wapo wachezaji wanaofanya vyema nje ya nchi lakini hawapati nafasi ya kuitwa timu za taifa kwa vile hawafuatiliwi kwa ukaribu na shirikisho la kandanda nchini.
"Nadhani kuna haja TFF ijenge utamaduni wa kuwafutilia wachezaji wao wanaocheza soka nje ya nchi kwa vile wapo wanaoweza kuwa msaada wa timu za taifa, lakini hawapati nafasi kwa vile hawafuatiliwi," alisema.
Alisema utamaduni wa kuwafuatilia wachezaji waliopo nje unaweza kuwa msaada mkubwa wa soka la Tanzania kwa sababu mchanganyiko huo unaweza kufanya Stars kuwa na kikosi imara.
Kwa sasa Stars imekuwa ikiwatumainia mchango wa nyota wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya DR Kongo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, huku wengine wakishindwa kuitwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kucheza ligi zisizo na umaarufu na kutofuatiliwa maendeleo yao.

No comments:

Post a Comment