Castor Mumbara alipokuwa akicheza 3 Star ya Nepal |
Timu hizo zitaumana kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika pambano la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Mumbara aliyewahi kuichezea timu za Moro Utd, Toto African, Yanga na Taifa Stars, alisema kujitokeza kwa wingi kwa mashabiki na kuiunga mkono Stars kuisaidia kupata ushindi dhidi ya wageni.
Alisema mbali na kuwahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi, pia aliwataka wachezaji wa Stars kuhakikisha wanapigana kiume uwanjani kuhakikisha wanaitoa kimasomaso Tanzania.
Mumbara aliyewahi kucheza soka la kulipwa katia klabu za 3 Star na Himalayan Sherpa, alisema kujituma kwa wachezaji uwanjani na mashabiki kuishangilia mwanzo mwisho kutaipa timu ushindi.
"Stars ikipewa sapoti na wachezaji wakijituma uwanjani inaweza kuwa silaha ya ushindi dhidi ya Morocco na kuisaidia kujiweka pazuri katika mbio za kwenda Brazil," alisema.Mumbara alisema Stars ina nafasi ya kwenda kwenye WC2014 iwapo itaungwa mkono mwanzo mwisho kwa mechi zilizosalia za kundi lake la C licha ya kuchuana na timu vigogo.
Stars inayoshika nafasi ya pili kwa sasa ikiwa na pointi tatu inahitaji ushindi Jumapili mbele ya Morocco ili kuzidi kuifukuzia Ivory Coast wanaoongoza kundi hilo kwa pointi nne ambapo Jumamosi itakuwa uwanjani kuumana na wanaoburuza mkia, Gambia.
Kikosi cha Morocco ambacho kitakuja bila nyota wake Marouane Chamakh anayekipiga West Ham kwa mkopo akitokea Arsenal kinatarajiwa kutua nchini kesho tayari kwa pambano hilo.
No comments:
Post a Comment