Yanga waliobanwa Morogoro |
Simba iliyobanwa Mwanza na Toto African |
Kagera imeilaza Mtibwa Sugar mabao 3-1 na kufikisha pointi 37 wakati Simba kwa sare hiyo ya Toto imefikisha pointi 35 na kutoa nafasi kwa Yanga na Azam kuzivua taji lake inalolishikilia kwa sasa.
Simba ilishtuliwa kwa bao la kuongoza la Toto lililofungwa dakika ya 25 kabla ya Simba kuchomoa dakika tatu baadaye kupitia ramadhani Mkopi na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe 1-1.
Kipindi cha pili Simba ilifunga bao la pili kupitia Mrisho Ngassa kabla ya Toto kusawazisha kupitia kwa Ramadhani na kufanya timu hizo zigawane pointi moja moja.
Yanga iliyokuwa mjini Morogoro ilishindwa kuivua Simba ubingwa na badala yake kutoa mwanya kwa Azam kuendelea kuwafukuzia katika mbio zao za kuwania taji la ubingwa msimu huu baada ya kulazimishwa suluhu ya kutofungana.
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoiengua Simba nafasi ya tatu |
Bao la Azam liliwekwa kimiani na kinara wa mabao wa Ligi Kuu kwa sasa Kipre Tchetche na kuifanya Azam kuiacha Simba kwa pointi 8.
Azam waliitungua Ruvu Shooting |
Jijini Dar es Salaam African Lyon imeiduwaza Coastal Union kwa kuilaza bao 1-0 wakati Arusha wenyeji, JKT Oljoro waliilaza maafande wenzao wa JKT Ruvu kwa mabao 2-0 na kuzidi kuimarisha mbio zake za kuelekea kwenye nafasi ya kuepuka kushuka daraja.
Matokeo kamili ya mechi za leo ni kama ifuatavyo hapo chini:
Polisi Moro v Yanga (0-0)
JKT Oljoro v Ruvu JKT (2-0)
Kagera Sugar v Mtibwa (3-1)
Toto African v Simba (2-2)
African Lyon v Coastal (1-0 )
Ruvu v Azam (0-1)
No comments:
Post a Comment