Ronaldo akishangilia bao lake la kwanza usiku wa jana |
MABINGWA
wa kihistoria wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid usiku
wa kuamkia leo imefuzu hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya mwaka huu
ikipokea kipigo ugenini cha mabao 3-2 toka kwa Galatasaray ya Uturuki.
Real
chini ya kocha wao Jose Mourinho walifanikiwa kufuau hatua hiyo kwa
faida ya mabao iliyopata katiika mechi ya nyumbani wiki iliyopita
walipoizima Galatasaray kwa mabao 3-0 hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao
5-3.
Nyota
wa klabu hiyo ya Hispania, Mreno Cristiano Ronaldo ndiye aliyesaidia
kuiokoa Real Madrid baa ya kufunga mabao mawili moja kila kipindi na
kusaidia kuivusha timu yake hatua hiyo.
Ronaldo
alifunga bao la kuongoza dakika saba tu ya mchezo huo uliochezwa
Uturuki na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe bao 1-0.
Kipindi cha pili wenyeji waliingia wakiwa wamecharuka na kusawazisha bao kupitia kwa Emmanuel Eboue katika dakika ya 57, kabla Wesley Sneijder hajaongeza bao la pili dakika ya 70.
Wesley Sneijder, akishangilia bao lake dhidi ya Real Madrid |
Katika dakika ya 72, Didier Drogba
aliifungia Galatasaray bao la tatu kabla ya Ronaldo kufunga goli la pili la kufutia machozi la Real Madrid dakika ya 90.
Katika
pambano jingine la michuano hiyo lililochezwa usiku wa jana nchini
Ujerumani wenyeji Borussia Dotmund walifanikiwa kusonga mbele kwenye
michuano hiyo baada ya kuwalaza wageni wao mabao 3-2.
Borussia Dortmund wakipongezana kufuzu nusu fainali dhidi ya Malaga |
Wageni
walionyesha kama wangewaadhiri wenyeji wao baada ya kutangulia kupata
bao dakika ya 25 kupitia Joaquin kabba ya Robert Lewandowski kusawazisha
dakika tano kabla ya mapumziko.
Eliseu
aliiongezea Malaga bao la pili dakika ya 82 na kuwafanya wageni hao
kuamini wamemaliza kazi katika pambano hilo kabla ya wenyeji wao
kucharuka na kuandika mabao mawili dakika za nyongeza.
Iliwachukua
dakika mbili tu za ziada kwa wenyeji hao kujipatia mabao hayo mawili
kupitia kwa Marco Reus kumalizia kazi nzuri ya Felipe Santana kabla ya
Santana kutupia la pili na kuwavusha mabingwa hao wa Ulaya wa mwaka 1997
kuungana na Real Madrid kucheza hatua ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment