Warembo wa Miss Utalii Tanzania na viongozi wao wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Chiku Galawa |
HATIMAYE fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,zinafanyika mkoani Tanga siku ya Jumapili katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga. Fainali hizo za tano za Taifa za mashindano ya Miss Utalii
Tanzania
tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, zitajumuisha jumla ya warembo 30 kutoka
mikoa yote ya Tanzania, na vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania taji la Taifa
la Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Zawadi
kwa mshindi wa kwanza ni mkataba wenye thamani ya sh.90, 000,000/=,ambao
unajumuisha schoolership ya kusoma kozi ya Diploma katika chuo cha Dar es Salaam
City Collage, safari za kushiriki mashindano ya Dunia,ziara za Tanzania Great
Safari and Tour 2013, kugharamiwa usafiri wakati wa shughuli za kutekeleza
majukumu yake ya ushindi,na shilingi 5,000,000/= baada ya kutumikia taji lake
wakati wa kukabidhi kwa mshindi wa msimu ujao.
Aidha
mshindi wa pili hadi wa tano, kila mmoja kila mmoja atajipatia mkataba wenye
thamani ya shilingi 58,000,000/=, ambao pia unajumuisha schoolership za kusoma
chuo cha Dar Es Salaam City Collage na safari za kushiriki mashindano ya
kimataifa nay a dunia, pia ushiriki wa safari za Tanzania Greet Safari and Tour
2013 na kugharamiwa usafiri wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya ushindi. Washiriki
walio bakia watajipatia tuzo mbalimbali za heshima, za utalii, utamaduni, jamii,
uchumi, mitindo, ,wanyama pori,misitu,mazingira,utalii wa ndani,utalii wa
kitamaduni,jinsia,utalii wa michezo,utalii wa mikutano,elimu ya jamii,afya ya
jamii, urembo na maliasili.
Mashindano
ya Dunia ambayo washindi hao watashiriki ni Miss Tourism World 2013, Miss
Tourism United Nation 2013, Miss Tourism University World 2013, Miss Heritage
World 2013, Miss United Nation 2013,Miss Freedom Of The World 2013,na Miss
Globe International 2013.
Burudani
katika fainali za mwaka huu ,zitakazo fanyika kitaifa mkoani tanga jumapili
tarehe 19-5-2013, ni pamoja na Bendi ya Msondo Ngoma, Mwana mziki wa kimataifa
Che Mundu Gwao, Ngoma za asili na vichekesho kutoka kundi la Majuto Arts Group
linalo ongozwa na mwigizaji mahili na mkongwe Mzee Majuto,sarakasi na muziki wa
kizazi kipya yani bongo fleva.Maandalizi yamekamilika, na hali ya kambi ni
shwari huku washiriki wote wakiwa katika hali ya kujiamini, kila mmoja
akijigamba kupeleka jaji mkoani kwake mwaka huu.
Katika
shindano la mwaka huu, katika ukumbi wa CCM Mkwakwani, wabunge ,madiwani,wakuu
wa wilaya,na viongozi wa vyama na serikali wamealikwa kuhudhuria. Mkuu wa mkoa
wa Tanga Mheshimiwa Chiku Galawa atakuwa mgeni rasmi katika fainaali hizo za
kihistoria kufanyika mkoani Tanga.
Tumepeleka
fainali za jumapili katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, ili kutoa fulsa kwa
wakazi wa kada zote kushudia fainali hizo, kwani shindano hili ni kwa ajili ya
watanzania wote bila kujali utofauti wao wa vipato wala umri,ndo mana viingilio
ni vya beii ya chini sana, ambapo shindano litaanza mchana wa saa 7 hadi usiku wa manane.
Viingilio watoto itakuwa 2000/=, wakubwa mzunguko itakuwa shilingi 5,000/=,
viti maalum shilingi 20,000/= na viti vya kawaida ni shilingi 10,000/=.
Shindano
la mwaka huu limedhaminiwa na asasi mbalimbali ikiwemo ya TANAPA BASATA, na wadhamini wengine.
No comments:
Post a Comment