Baadhi ya askari polisi wakionyesha kwa waandishi wa habari silaha zilizokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa matukio ya ujambazi.
DCP Mlege akitoa taarifa ya mafanikio ya
Jeshi hilo kwa waandishi wa habari ambapo akizungumzia suala la Mh.
Mnyika amesema askari No. E. 5340 D/CPL Julius aliyekuwa ndani ya gari
la polisi PT. 1902 alikuwa anasogeza boksi lenye mabomu ya kutoa machozi
ya kurusha kwa mkono, kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya
gari hilo na halikuleta madhara yeyote kwa askari polisi wala raia
waliokuwa eneo la uwanja wa Sahara uliopo Mabibo ambako chama cha
CHADEMA kilikuwa kifanye mkutano wa hadhara tarehe 21 Jula 2013 kinyume
na utaratibu.
Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata sila 5
ikiwemo SMG moja, Shortgun mbili, Riffle Mark 3 tatu, Pisto moja, Risasi
56, Maganda ya Risasi 17 na Majambazi 8.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya
Kamishna wa polisi kanda hiyo, DCP A.M. Mlege amesema zoezi hilo
lilifanyika Julai 18 mwaka huu katika maeneo ya Magomeni wilaya ya
Kinondoni.
Amesema pia Jeshi hilo limeweza kukamata magari ya wizi matano, Injini
tatu za magari, Vipande vya magari yaliyokatwa spea na wezi watano wa
magari.
Katika hatua nyingine Jeshilo limekanusha habari zilizotolewa katika
vyombo vya habari kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika kukoswa
na bomu na kumjeruhi mmoja wa wafuasi wake.
Aidha limeomba siku zingine kabla ya kutoa habari ni vizuri likaulizwa ili kuthibitisha au kukanusha.
DCO Mlege amesema pia Jeshi la polisi Kanda maalum Dar es Salaam
limemkamata tapeli hatari anayetumia namba tofauti za mitandao ya simu
na majina ya watu maarufu anajulikana kwa jina la Mfaume Omari maarufu
kama ‘Mau’.
Chanzo - MOBLOG
No comments:
Post a Comment