Athuman Rupia (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya wavu |
Michuano hiyo ya Kanda ya Tano Afrika, inafanyika nchini Uganda kwenye uwanja wa MTN Sports uliopo Lugogo jijini Kampala ikishirikisha timu nne wakiwamo wenyeji Uganda.
Kwa mujibu wa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, Athuman Rupia aliyezungumza na MICHARAZO kwa njia ya simu asubuhi hii kutoka Uganda, ni kwamba Tanzania ilishindwa kufuruka kwa Wakenya kutokana na hali ya uchovu waliokuwa nao baada ya kutua nchini humo majira ya asubuhi na jioni kushuka dimbani.
"Tumeanza vibaya michuano ya Kanda ya Tano kuwania Fainali za Kombe la Dunia baada ya kufungwa sti 3-0 na Wakenya, ila tunaamini uchovu umechangia kipigo chetu na tunajipanga kwa mechi zilizosalia dhidi ya Burundi na wenyeji Uganda," alisema Rupia anayeichezea pia timu ya Jeshi Stars.
Jumla ya timu za taifa za nchi nne tu kati ya sita zilizotarajiwa kushiriki michuano hiyo ndizo zinazochuana jiji Kampala baada ya wakali kutoka Sudan na Rwanda kujioengua dakika za lala salama na kuziacha Kenya, Uganda, Tanzania na Burundi zikionyeshana kazi kuwania nafasi tatu za Kanda hiyo ya Tano.
No comments:
Post a Comment