Kocha Jose Mourinho akionesha ishara ya busu kwa mashabiki wa Chelsea waliofurika Stamford Bridge
Oscar akishangilia bao lake
Mfungaji wa bao la pili la Chelsea akiwajibika uwanjani.
KOCHA
wa Chelsea , Mreno, Jose Mourinho ameanza kwa kishindo Stamford Bridge
tangu arejea kwa mara ya pili baaada ya kuibuka na ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya timu mpya ya ligi kuu soka nchini England, Hull City.
Ikiwa
imepita takribani miaka sita tangu aondoke darajani na kurejea majira
haya ya kiangazi, leo hii Mourinho alianza kibarua katika dimba la
nyumbani na kushangiliwa na mashabiki lukuki wanaomuunga mkono kwa
asilimia mia moja.
Katika
mchezo huo, kiungo mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard alikosa mkwaju wa
penati dakika ya sita baada ya kipa wa Hull, Allan McGregor kuokoa na
baada ya hapo kipa huyo aliokoa tena mpira wa kichwa uliozamishwa na
Branislav Ivanovic , lakini teknolojia ya goli iligoma na kuwaambia
Chelsea sio goli.
Bao
la kwanza la Chelsea lilifungwa na Oscar katika dakika ya 13 akipokea
pasi ya mwisho kutoka kwa Kevin de Bruyne, na bao la pili limefungwa na
Frank Lampard dakika ya 25 na kufuta makosa ya kukosa penati.
Katika pambano jingine ;a mapema jana, Tottenham wakiwa ugenini waliipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Bao pekee lililoipa vijana wa Spurs ushindi huo lilifungwa na mchezaji mpya wa timu hiyo Roberto Saldado kwa njia ya penati dakika ya 50.
No comments:
Post a Comment