WaFUASI wa Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda wamepiga kambi katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam wakitaka kumwona bila mafanikio.
Wakizungumza jana nje ya gereza hilo, wafuasi hao
walisema walipofika hapo saa nne asubuhi waliambiwa kwamba tayari ndugu
zake wanne walikwisharuhusiwa kuingia kumwona.
“Tumeambiwa kwamba idadi watu hao inatosha na kwamba wengine haturuhusiwi kumwona,” alisema mmoja wa wafuasi hao, Baraka Mohamed na kuongeza: “Tunaendelea kusubiri huruma za askari wa Magereza labda baadaye wanaweza kuturuhusu kumwona,” alisema.
Wafuasi hao ambao walijaza sehemu kubwa ya eneo la
mapokezi na nje ya gereza hilo walilalamikia kitendo cha askari hao
kutokuwaruhusu kumwona kiongozi wao.
“Nimefika hapa asubuhi na mapema, lakini utaratibu
sikuupenda kwa kweli. Nimezuiwa nami nataka kumwona kiongozi wangu na
si mimi tu tuko wengi hapa,” alisema mfuasi huyo.
Wafuasi hao hawakukata tamaa kwani licha ya
kuzuiwa waliamua kukaa jirani na lango la gereza na wengine kusimama
vikundi vikundi wakijadiliana namna ya kupata nafasi ya kumwona. Sheikh
Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili
(Moi) alipelekwa katika gereza hilo Alhamisi iliyopita.
Hatua hiyo ilikuja baada ya kusomewa shtaka la
uchochezi akiwa kitandani akidaiwa kutenda kosa hilo katika maeneo
mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 hadi Agosti
11 mwaka huu.
Kwa nini walizuiwa?
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Deodatus
Kizinja alisema jana kuwa kisheria ni watu wawili katika kipindi cha
wiki nne wanaoruhusiwa kumwona kila mahabusu.
Hata hivyo, alisema kwa kuzingatia sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na wananchi, wamekuwa wakiruhusu idadi zaidi kila inapobidi.
“Kwa watu maarufu kama Ponda, Jeshi la Magereza
linakuwa makini kudhibiti umati wa watu wanaotaka kumwona mahabusu kwa
sababu hatuwezi kufahamu kama watu wote wana nia njema au la,” alisema
Kizinja na kusisitiza kuwa ndugu zake wanne ambao walishaingia kumwona
wanatosha.
Lipumba ataka afutiwe mashtaka
Pia amelaani kitendo cha polisi kumwondoa Sheikh Ponda hospitali na kumpeleka gerezani huku akiwa bado anaendelea na matibabu ya jeraha alilopata.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema: “Tunaitaka Serikali ifute makosa yote ya uchochezi aliyopewa Sheikh Ponda... kwani siku zote inafahamika mtu akisema ukweli anaonekana mchochezi.”
Waumini walia na Nchimbi, Shilogile
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam walisema viongozi hao wameshindwa kuchukua hatua stahili kwa polisi waliohusika kumdhuru Sheikh Ponda.
Sheikh Ponda anadaiwa kupigwa risasi na polisi mjini Morogoro Agosti 10, mwaka huu.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wafuasi wake, viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania walieleza kutokufurahishwa na jinsi Jeshi la Polisi lilivyoshughulikia suala la Sheikh Ponda.
Mwakilishi wa Jumuiya hiyo, Sheikh Kondo Juma alisema Dk Nchimbi na Shilogile wanapaswa kuachia ngazi kutokana na kumbambikia kesi Sheikh Ponda.
Sheikh Juma alisema mbali na kutaka Shilogile ajiuzulu, alitaka kamanda huyo afikishwe mahakamani kutokana na Sheikh Ponda kujeruhiwa.
CCM waombe radhi
Msemaji wa Familia ya Ponda, Isihaka Rashid alisema alikwenda
katika gereza hilo kumwona kiongozi huyo Jumamosi iliyopita lakini
alizungumza naye kwa muda mfupi akaomba akapumzike...
“Jumamosi iliyopita tulimpelekea dawa, tukazungumza naye kwa muda mfupi akaomba akapumzike kwa sababu bado alikuwa anasikia maumivu,” alisema.
“Jumamosi iliyopita tulimpelekea dawa, tukazungumza naye kwa muda mfupi akaomba akapumzike kwa sababu bado alikuwa anasikia maumivu,” alisema.
Lipumba ataka afutiwe mashtaka
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
ameitaka Serikali imfutie kesi ya uchochezi Sheikh Ponda kwa madai kuwa
ni ya kubambikiziwa.
Pia amelaani kitendo cha polisi kumwondoa Sheikh Ponda hospitali na kumpeleka gerezani huku akiwa bado anaendelea na matibabu ya jeraha alilopata.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema: “Tunaitaka Serikali ifute makosa yote ya uchochezi aliyopewa Sheikh Ponda... kwani siku zote inafahamika mtu akisema ukweli anaonekana mchochezi.”
Waumini walia na Nchimbi, Shilogile
Wafuasi wa Sheikh huyo wamepanga kuandamana nchi
nzima kushinikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile waachie
ngazi.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam walisema viongozi hao wameshindwa kuchukua hatua stahili kwa polisi waliohusika kumdhuru Sheikh Ponda.
Sheikh Ponda anadaiwa kupigwa risasi na polisi mjini Morogoro Agosti 10, mwaka huu.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wafuasi wake, viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania walieleza kutokufurahishwa na jinsi Jeshi la Polisi lilivyoshughulikia suala la Sheikh Ponda.
Mwakilishi wa Jumuiya hiyo, Sheikh Kondo Juma alisema Dk Nchimbi na Shilogile wanapaswa kuachia ngazi kutokana na kumbambikia kesi Sheikh Ponda.
Sheikh Juma alisema mbali na kutaka Shilogile ajiuzulu, alitaka kamanda huyo afikishwe mahakamani kutokana na Sheikh Ponda kujeruhiwa.
“Hawa viongozi wawili wanapaswa kuwajibika. Tutaandaa maandamano
nchi nzima ili kushinikiza wajiuzulu,” alisema Sheikh Juma kwenye
mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,
Englebert Kiondo.
Sheikh Juma alieleza kuwa ikiwa viongozi hao wataendelea kushikilia nafasi hizo, watakinyima kura CCM mwaka 2015.
CCM waombe radhi
Akizungumza katika mkutano huo, Kiongozi wa
Kiislamu kutoka Zanzibar, Sheikh Salum Amour aliitaka Serikali ya CCM
kuomba radhi kutokana na suala la Sheikh Ponda kuhusishwa na matukio ya
umwagaji wa tindikali.
Pia alitishia kuwa isipoomba radhi, watainyima kura CCM kwenye uchaguzi ujao.
Mwananchi
Mwananchi
No comments:
Post a Comment