Amani Simba |
Aidha kipa huyo alisema ni mapema mno kuanza kuitabiria ligi ya msimu huu kwa sababu anaamini lolote linaweza kubadilika kwa sasa kutpkana na ukweli ligi ndivyo kwanza ipo raundi ya nne kwa sasa.
Simba aliyeidhinishwa hivi karibuni na TFF kuidakia timu hiyo baada ya kuitema timu aliyoipandisha daraja ya Mbeya City, alisema Ashanti inasumbuliwa na ugeni wa ligi, ila kadri siku zinavyosonga mbele wachezaji wataizoea na kutisha.
Kipa huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Moro United, Simba na Taifa Stars alisema ni mapema mno kuanza kuihukumu Ashanti na matokeo iliyopata kwa sasa kwa sababu ligi bado mbichi na wachezaji wao wanaendelea kuizoea ligi hiyo.
"Ni mapema mno kuijadili Ashanti, naamini muda mfupi ujao wanayoibeza wataikubali baada ya kuanza kupata matokeo mazuri, unajua ugeni wa ligi ndiyo tatizo lakini kadri siku zinavyoenda mbele wachezaji wanaondoa woga," alisema.
Simba, aliyewahi pia kuzidakia Lipuli Iringa, Prisons Mbeya na JKT Ruvu, alisema akishirikiana na wenzake watahakikisha Ashanti inafanya vyema katika mechi zilizopo mbele yake.
Ashanti United inayoburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa pointi moja ni kati ya timu tatu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, nyingine zikiwa ni Mbeya City na Rhino Rangers ya Tabora.
No comments:
Post a Comment