STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 24, 2013

Jeshi Kenya lakaribia kumaliza kazi yaua magaidi 9

NAIROBI

JESHI la Kenya limedaiwa limedhibiti kwa asilimia kubwa jengo la Westgate, ikidaiwa wamewaua magaidi 9 na kuhisiwa gaidi mmoja au wawili tu ndiyo waliosalia kwenye jengo hilo na wakati wowote watashughulikiwa na kumaliza utekaji wa siku nne sasa.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na AFP, inasema kazi kubwa ya kupambana na magaidi hao kutoka kikundi cha Al Shabaab cha Somalia, wamefanikiwa kulidhibiti jengo hilo baada ya mapambano makali ya siku mbili mfululizo.
Mirushiano ya risasi baina ya pande hizo mbili zimepungua kwa hivi sasa kulingana na hali ilivyokuwa jana, ambapo pilikapilika zilikuwa za kutosha huku watu wakiwa na taharuki.
Hata hivyo mpaka sasa bado taarifa zinasema waliofariki katika tukio hilo ni watu 62 na wengine 63 hawafahamiki walipo huku watu zaidi ya 200 wakiwa wamejeruhiwa japo baadhi yao wametibiwa na kuruhusiwa kurudi majumbani mwao.
Muda mchache uliopita imeripotiwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Kenya, Jomo Kenyatta alikuwa akijiandaa kulihutubia taifa kuwapa ukweli wa tukio hilo na takwimu halisi la operesheni hiyo ambayo imefanikishwa na vikosi vya ulinzi na usalama wa nchini hiyo ya Afrika Mashariki.
Magaidi hao wa Al Shaaban waliojinasibu kuhusika na tukio hilo walivamia jengo hilo lenye maduka ya bidhaa mbalimbali na kuwafyatulia risasi wateja na watumishi wa maduka hayo siku ya Jumamosi na kusababisha maafa hayo makubwa.
Hili ni tukio kubwa kufanywa na kundi hilo linalodaiwa linafadhiliwa na Al Qaida baada ya lile la mwaka 2010 mjini Kampala, Uganda wakati mashabiki wa soka zaidi ya 70 kulipuliwa kwa mabomui wakati wakiangalia Fainali za Kombe la Dunia katika runinga.
Msemaji wa kundi hilo alinukuliwa juzi kubwa wamefanya mauaji hayo kushinikiza serikali ya Kenya kuliondoa jeshi lake nchini Somalia wanapolinda amani katika jeshi la Umoja wa Mataifa, kitu ambacho serikali ya Nairobi imesisitiza hawataondoa jeshi lao.

No comments:

Post a Comment