WAUAJI wawili wa kujitoa mhanga wamelipua mabomu yao nje ya kanisa la
kihistoria nchini Pakistan jana na kuua watu 75 kwenye shambulio baya
zaidi kuwahi kutokea kwa Wakristo walio wachache wa nchini humo.
Taliban wa Pakistan wamekiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea katika mji wa Peshawar, wakisema wataendelea kuwalenga wasio Waislamu hadi hapo Marekani itakapositisha mashambulizi katika mji huo wa kikabila nchini humo.
Shambulio la hivi karibuni lilifanyika Jumapili pale makombora yalipopiga majengo mawili katika eneo la North Waziristan, na kuua watu sita wanaodhaniwa kuwa wanamgambo, maofisa wa intelijensia Pakistan walisema.

Shambulio kwenye Kanisa la All Saints, ambalo pia lilijeruhi watu 110,
linatekeleza kitisho kilichotolewa na Taliban wa Pakistan wakati huku
serikali ikitaka mpango wa amani na wanamgambo hao.
Shambulio hilo limetokea wakati mamia ya waumini wakiwa wanatoka nje ya
kanisa hilo lililoko katika wilaya ya Kohati Gate mjini humo baada ya
huduma ya kupata chakula cha bure aina ya wali.
"Kulikuwa na milipuko na kulikuwa na mateso kwetu sote," alisema Nazir
John, ambaye alikuwa kanisani pamoja na takribani waumini wengine 400.
"Niliporejewa na fahamu zangu, sikuona chochote ila moshi, vumbi, damu
na watu waliokuwa wakilia kwa uchungu. Niliona sehemu za miili
zilizosambaratika na damu kuzunguka eneo lote."
Manusura walikumbatiana kila mmoja baada ya milipuko huko.
Ukuta mweupe wa kanisa hilo, ambalo lilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa miaka ya 1800, ulitapakaa mashimo yaliyochimbwa na vipande vya vyuma vilivyotoka katika mabomu ma kusababisha uharibifu mkubwa.

Damu ilitapakaa sakafuni na kusambaa kwenye ukutani. Sahani zenye wali zilitawanyika kila pembe za eneo hilo.
Shambulio hilo lilifanywa na watuhumiwa wawili wa kujitoa mhanga ambao
walilipua mabomu yao kwa kupokezana. Mamlaka zimekuta sehemu za mwili na
zilikuwa zikijaribu kutambua umri wao.
Milipuko hiyo imeua watu 75 na kujeruhi wengine 110. Waliokufa ni pamoja na wanawake na watoto.
Idadi ya majeruhi ni kubwa mno kiasi cha hospitali hiyo kuishiwa
majeneza kwa ajili ya waliokufa na vitanda kwa ajili ya majeruhi,
alisema Mian Iftikhar Hussain, waziri wa zamani wa habari wa jimbo la
Khyber Pakhtunkhwa ambaye alikuwa katika eneo la tukio.
"Hili ni shambulio baya zaidi dhidi ya Wakristo katika nchi yetu," alisema Irfan Jamil, askofu wa mji wa mashariki wa Lahore.
Mmoja wa waliojeruhiwa, John Tariq, ambaye amepoteza baba yake katika
shambulio hilo, aliwauliza washambulizi hao, "Tumewakosea nini watu
hawa? Kwanini tumekuwa tukiuawa?"
Ahmad Marwat, ambaye alijitambulisha kama msemaji wa tawi la Jundullah
la Taliban wa Pakistan, alidai kuhusika na shambulio hilo.
"Wote wasio Waislamu nchini Pakistan ni walengwa wetu na wataendelea
kuwa hivyo kwa wakati wote Marekani inaposhindwa kusitisha mashambulizi
katika nchini yetu," alisema Marwart kwa njia ya simu kutoka sehemu
isiyojulikana.
Askofu wa Peshawar, Sarfarz Hemphray, ametangaza siku tatu za maombolezo
kufuatia shambulio hilo na kuishutumu serikali na vyombo vya ulinzi kwa
kushindwa kuwalinda Wakristo wa nchini humo.
"Endapo serikali itaonesha nia, inaweza kudhibiti ugaidi huu," alisema
Hemphray. "Tumekuwa tukizitaka mamlaka kuimarisha ulinzi, lakini
hazitilii maanani."
Waziri Mkuu wa Pakistani ameshutumu shambulio hilo katika taarifa
iliyotumwa kwa waandishi wa habari, akisema, "Magaidi hawana dini na
wanaolenga watu wasio na hatia ni kinyume cha mafundisho ya Kiislamu na
dini zote."
"Matukio kama hayo ya kiwendawazimu ya ugaidi yanaakisi unyama na akili zisizo za kibinadamu za magaidi," alisema.
No comments:
Post a Comment