Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah akiongea wakati wa halfa hiyo.
|
Mkurugenzi
wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya
wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.
Tanzania waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.
Katika pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni Shelda Boniface na mvulana ni Athanas Mdamu na pia amempongeza mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .
Katika mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande wa wasichana magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne , mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na kuondoka na mpira kila mmoja.
Kabla ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao, Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini, bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.
Akiongea kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa , amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na DRFA
Mkurugenzi wa masoko wa Airtel bw Levi Nyakundi ameahidi kuwa Airtel itaendelea kudhamini mpira hasa wenye umri mdogo na pia kuongeza mikoa ya ushiriki wa mashindano ya Airtel Rising Stars.

No comments:
Post a Comment