WATEMBEA kwa miguu wawili wamepotea maisha yao baada ya kugongwa na gari lililoacha njia mjini Mbeya huku watu wengine wawili wakinaswa na dawa za kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa gramu 900.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Polisi mjini humo inayosemeka hapo chini ni kwamba watu hao walipatwa na ajali hiyo jana saa 1 usiku. Isome mwenyewe taarifa hiyo.
MNAMO
TAREHE 03.10.2013 MAJIRA YA SAA 19:46HRS HUKO KATIKA ENEO LA SIMIKE JKT – ITENDE BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI
T.170 AUM AINA YA TOYOTA CRESTA
LIKIENDESHWA NA DEREVA MAHUNDI S/O
KAPITI, MIAKA 27, KYUSA, MKAZI WA ITIJI LILIACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA
KWA MIGUU WAWILI KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA
VIFO VYA WATU WAWILI AMBAO NI 1. DEREVA
MWENYEWE 2. NEEMA D/O MWINUKA,
MIAKA 32, MNDALI, MWALIMU AMBAYE ALIKUWA MTEMBEA KWA MIGUU MKAZI WA NZOVWE PIA
KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WAWILI AMBAO NI 1.TWINZA S/O MWAKIYOMA, MIAKA 36, KYUSA, MKAZI WA MAJENGO AMBAYE
AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA 2. STIVIN S/O MWAKALINGA, MIAKA 36,
KYUSA, MKAZI WA NZOVWE AMBAYE ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. CHANZO NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
|
WILAYA
YA MOMBA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 03.10.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS
HUKO KATIKA MTAA WA MAPOROMOKO TUNDUMA WILAYA
YA MOMBA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. IZDORI
S/O PELLA, MIAKA 24, MKINGA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MAPOROMOKO NA 2. AMOS S/O ALISON MELLA, MIAKA 28, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI
WA MTAA WA MIGOMBANI WAKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 900. MBINU NI KUFICHA
BHANGI HIYO KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA IZDORI S/O PELLA. WATUHUMIWA NI
WAVUTAJI NA WAUZAJI WA BHANGI. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU
WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA AZITOE KWENYE MAMLAKA
HUSIKA ILI WAKAMATWE.
Signed
by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment