Julio akitetea na Mombeki na Henry Jospeh akiwa kando yake |
Hata hivyo kitu cha kufurahisha ni kwamba nahodha wake msaidizi, Nassoro Masoud 'Chollo' na mkongwe Henry Joseph wenyewe wapo fiti tayari kuwakabili maafande hao wanaonolewa na kocha Charles Boniface Mkwasa.
Akizungumza na MICHARAZO kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema Simba ipo kamili kuivaa Ruvu licvha ya kuwakosa Abdallah Seseme na Miraji Adam ambao wote wamefungwa plasta gumu (POP) miguuni.
Julio alisema ukiondoa wachezaji hao wengine wanaendelea vyema japo hali ya Baba Ubaya aliyeanza mazoezi na wenzake bado haijatengemaa vizuri na hivyo kutokuwa na hakika ya kumtumia katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa na kudai itakuwa ngumu na yenye ushindani mkubwa.
"Kikosi kipo tayari kwa vita dhidi ya Ruvu Shooting, japo tunasikitika kusema kuwa hatutakuwa na Seseme na Miraj ambao wote wamefungwa POP huku Baba Ubaya akitupa mashaka, japo Henry Joseph na Chollo wamerejea dimbani kuungana na wenzao ambao wana ari ya ushindi," alisema.
Kuhusu mfungaji wao bora, Amisi Tambwe ambaye majuzi alishindwa kuendelea na mazoezi na wenzake kutokana na kusumbuliwa na tumbo, Julio alisema anaendelea vyema na Jumamosi ataendelea kuongoza 'mauaji' kwa Ruvu.
"Aaah alichafukwa na tumbo tu na wala halikuwa tatizo kubwa na panapo majaliwa ataendelea kuongoza mauaji dhidi ya wapinzani wetu katika Ligi Kuu," alisema Julio beki wa zamani wa Plisner, Simba na Taifa Stars.
Mbali na mechi ya Simba na Ruvu, kesho kutakuwa na mechi nyingine nne zitakazozikutanisha timu za JKT Ruvu dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Chamanzi, Coastal Union kuialika Azam jijini Tanga na Oljoro JKT kuikaribisha Mbeya City kabla ya Jumapili Yanga kupepetana na Mtibwa Sugar na Mgambo JKT kuumana na Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga
No comments:
Post a Comment