Golden Bush iliyopanda Daraja hadi la Tatu Kinondoni |
TIMU ya soka ya Golden Bush Fc iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Nne Wilayani Kinondoni, imefanikuwa kupanda daraja hadi la Tatu.
Golden Bush klabu mpya katika na iliyokuwa ikishiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza imefuzu daraja la tatu kutokana na kufanya vyema katika mechi zake za mzunguko wa pili.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa klabu hiyo ni kwamba Chama cha Soka wilayani humo (KIFA) imeitangaza klabu hiyo kupanda daraja.
MICHARAZO inawapa pongezi vijana hao kwa mafanikio hayo na ikiwakumbusha hawapaswi kuvimba kichwa badala yake ijipange kukabiliana na michuano iliyopo mbele yao;
Taarifa hiyo ya uongozi wa Golden Bush unasomeka hapo chini kama ifuatavyo, l
Wadau,
Nimekuwa
kimya kwa muda mrefu hii inatokana na majukumu kuingiliana kidogo na
kukosa muda wa kuwalisha taarifa mpyampya. Leo napenda niwataarifu
kwamba ile timu yetu ya vijana imetangazwa rasmi na KIFA kwamba imepanda
daraja la tatu. Hii imetokana na kumaliza mzunguko wa mwisho bila
kutoteza mechi hata moja. mimi binafsi nilibahatika kuangalia mechi kama
tatu hivi vijana wakifanya mamabo mazito, hakika mpira ni maandalizi na
siyo kununua refa. Tumecheza games zote bila kumpa hata shilingi 500
refa nab ado tumefanilkiwa kumaliza ligi katika mzunguko wa pili ambao
ni mgumu kabisa bila kufungwa.
Binafsi
nawapongeza sana vijana kwa kazi kubwa sana lakini pongezi za pekee
wanastahili bench la ufundi chini ya Madaraka Selemani, Katina Shijja
na Waziri Mahadhi kwa matokeo mazuri na kupandisha timu daraja ambayo
kwa sasa hivi imekuwa gumzo hapa Dar es Salaam. Aidha ningependa
kuwopongeza kwana namna ya pekee kabisa wachezaji wa timu yetu ya
Veterans kwa msaada mkubwa wa kiushauri kwa mudawao wa kujitolea kutoa
mawazo ya kila aina ambayo kwa hakika ndiyo yametufanya tufika hapoa
tulipo leo. Nakumbuka hatua ya kwanza kabisa tulifungwa game ya kwanza
1-0, baada ya kupata matokeo yale wazee waliwaita vijana na kuwapa
ushauri wa kisaikolojia, kiufundi na kuwaandaa kitalaam kabisa kwa game
iliyofuata, nakumbuka tulishinda mecho zote zilizofuata na kuna timu
ilikimbia baada ya kuona hadi half time tumewapiga 7-0. Nawashukuru sana
watu wazima wakiongozwa na Macocha kwa kazi nzuri nzuri nzuri sana. Ni
furaha kubwa nay a pekee unapokuwa na timu inayoandaliwa kucheza mpira
siyo kwenda kuloga na kuhonga marefa. Tumefanya kazi yetu na wote kwa
pamoja tunastahili sifa na kujipongeza.
Golden bush oyeeeeeeeeee!
No comments:
Post a Comment