Daniel Sturridge akiifungia Liverpool bao la pili jioni ya leo (Picha: Peter Byrne, PA Wire) |
WAKATI Liverpool ikizidi kupepea kwenye Ligi Kuu ya England (EPL), Manchester City jioni ya leo imezinduka baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Everton.
City waliofungwa mabao 3-2 katika mechi yao iliyopita ya EPL dhidi ya Aston Villa kabla ya kulazwa mabao 3-1 na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya , leo ikiwa kwenye uwanja wake wa Etihad, iliwakimbizaa Everton na kupata ushindi huo uliowapeleka hadi kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.Mabao ya Negredo, Sergio Aguero na lile la kujifunga la Tim Howard yalitosha kuwafanya mabingwa hao wa zamani wa England kupumua kwa muda, huku Romeu Lukaku akiendelea kufumania nyavu akifikisha bao la nne katika mechi zake nne kwa kuifungua Everton bao la kufutia machozi katika mechi hiyo.
Nayo Liverpool imekwea hadi nafasi ya kwanza baada ya kuifunga Crystal Palace mabao 3-1 kwenye uwanja wa Anfield.
Mabao ya washindi yalitupiwa kimiani na Luis Suarez, Daniel Sturridge na penati ya nahodha Steven Gerrard na kutosha kuipa uongozi wa ligi hiyo ya England ikiwa na pointi 16, moja zaidi ya ilizonazo Manchester City na Arsenal waliopo nyuma yao.
Katika mechi nyingine Newcastle United ikiwa ugenini iliifumua Cardiff City kwa mabao 2-1, huku Fulham kipata ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Stoke City, nayo Hull City na Aston Villa zikishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu ya ila kufungana.
Muda mchache ujao timu ya Manchester United itashuka ugenini kukabiliana na 'vibonde' wa ligi hiyo Sunderland.
No comments:
Post a Comment