JKT Ruvu waliozinduka leo |
Mbeya City waliotaka jijini Arusha |
Coastal waliobanwa mbavu na Azam |
Mbeya iliypanda daraja msimu huu toka Daraja la Kwanza huo ni ushindi wake wa pili na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 11 kutokana na mechi saba ilizocheza mpaka sasa.
Wakali hao toka Mbeya walipata mabao yake kupitia kwa Paul Nonga na Peter Mapunda aliyefunga dakika mbili kabla ya pambano kumalizika, huku bao la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Expedito Kiduko.
Nayo JKT Ruvu iliyokuwa imesimamishwa kwa muda mrefu kuendelea na wimbi lake la ushindi kwa kupokea vipigi vitatu mfululizo, leo iliamka uwanja wa Chamazi wa kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1.
Mabao ya Machaku Salum na Bakar Kondo yalitosha kuzima kasi ya Kagera ambayo walikuwa wakiifukizia Simba kileleni huku bao la kufutia machozi la wana Nkurukumbi likifungwa na Themi Felix.
Ushindi huo wa maafande hao wa JKT Ruvu umeifanya kuwekea hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 12 na kuiengua Kagera katika nafasi hiyo, ikitofautiana na vinara wa ligi hiyo kwa pointi tatu. Simba kwa sare ya leo dhidi ya Ruvu Shooting imefikisha jumla ya pointi 15.
Katika mechi nyingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga mdudu wa sare ameendelea kuziandama timu za Azam na Coastal Union baada ya timu hizo kushindwa kutambiana na kutoka suluhu ya kutokufungana.
Ligi hiyo ya Vodacom, itaendelea kesho kwa mechi mbili ambapo mabingwa watetezi Yanga wataikaribisha Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Taifa, wakati Mgambo JKT wakiwa mjini Tanga watapepetana na maafande wenzao wa Prisons-Mbeya.
No comments:
Post a Comment