TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Mhandisi (Eng.) Bashir J. Mrindoko kuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maji kwa kumpandisha cheo kutoka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Mhandisi Mbogo Paulo Futakamba, Naibu KatibuMkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwenda Wizara ya Maji kujaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Bashir Mrindoko.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Jumanne, Oktoba 15, 2013, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa vile vile Rais Kikwete amemteua Mhandisi Raphael Leyan Daluti kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuchukua nafasi ya Mhandisi Futakamba.
Kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Daluti alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji na Huduma za Ufundi katika Wizara hiyo ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Balozi Sefue amesema katika taarifa yake kuwa uteuzi na uhamisho huo umeanza Oktoba 13, mwaka huu, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Oktoba, 2013

No comments:
Post a Comment