Kikosi cha Ashanti United |
LIGI
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Oktoba 16 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ashanti United na Tanzania
Prisons itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Nayo
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea kesho (Oktoba 16 mwaka huu)
kwa mechi moja ya kundi A ambapo Polisi Dar es Salaam itakuwa mwenyeji
wa Tessema kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekabidhi kitanda cha upasuaji kwa
Hospitali ya Rufani ya Manispaa ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya mchango
wake kwa jamii.
Makabidhiano
hayo yamefanyika leo (Oktoba 15 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa
TFF ambapo Hospitali ya Temeke iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
hospitali hiyo James Syaga, Mganga Mkuu Dk. Amaani Malima na Matroni wa
hospitali hiyo Deodata Msoma.
Akikabidhi
kitanda hicho chenye thamani ya sh. milioni 6.8, Katibu Mkuu wa TFF,
Angetile Osiah alisema amefurahi kuwa ahadi ya kukabidhi msaada huo wa
Hospitali ya Temeke umetimia licha ya kuchukua muda mrefu kutokana na
ukweli kuwa fedha za kununulia kitanda hicho zinatokana na mchezo wa
Ngao ya Jamii wa mwaka jana kati ya Simba na Azam FC.
Alisema
uamuzi wa kuiteua Hospitali ya Temeke ulitokana na ukweli kuwa pamoja
na kwamba ofisi za TFF ziko wilayani Ilala, shughuli nyingi kubwa za
Shirikisho linafanyika kwenye Manispaa ya Temeke na hivyo hospitali hiyo
hufanya kazi kubwa ya kuhudumia watu mbalimbali wanaopata matatizo
wakati wa michezo ya mpira wa miguu.
Naye
Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Malima aliishukuru TFF kwa kutimiza ahadi
yao na kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa wana vyumba
vitatu vya upasuaji, lakini ni viwili tu vilivyo na vitanda kwa hiyo
kitanda hicho kitakamilisha chumba hicho kianze kufanya kazi.
Alisema
Hospitali yake sio tu inahudumia wagonjwa kutoka wilayani Temeke, bali
kutoka hata Mkoa wa Mtwara na sehemu nyingine zinazozunguka wilaya hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Hospitali, James Syaga, ambaye alisema anawakilisha watu
wanaohudumiwa na Hospitali ya Temeke, alishukuru kwa msaada huo na
kuiomba TFF kuendelea kuangalia uwezekano wa kusaidia hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment