Kelvin Nyoni 'K Guitar' kaika pozi |
Tayari wimbo huo umeanza kurushwa hewani na baadhi ya vituo vya redio nchini na kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kufyatua video yake ili mashabiki wapoate uhondo kamili.
Akizungumza na MICHARAZO, mwanamuziki huyo anayecharaza pia gitaa la rythm alisema wimbo huo ameurekodia katika studio za Swadt Records chini ya prodyuza T-Tach kwa msaada mkubwa wa mameneja wake watatu akiwamo mchora katuni wa gazeti hili, Abdul King'O.
Kelvin alisema wimbo huo ni mwanzo wa safari ndefu ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki kupitia albamu yake binafsi itakayokuwa na nyimbo zaidi ya sita katikka miondoko tofauti za Zouk, Bongofleva na Rhumba.
"Baada ya kukamilisha kutoa video ndipo nitaanza kurekodi nyimbo nyingine ambapo mpaka sasa tayari ninazo kama tatu zilizokamilisha mashairi yake," alisema Kelvin.
Kelvin kabla ya kuingia kwenye muziki wa dansi akijiunga na bendi ya Bana Marquiz inayoongozwa na mwanamuziki nyota wa kimataifa, Tshimanga Assosa Kalala 'Mtoto Mzuri', alishawahi kutoa wimbo wa Bongofleva wa 'Mapenzi Siyo Pesa' kabla ya kuurudia tena katika bendi hiyo.
No comments:
Post a Comment