Michuano
ya Kombe la Uhai imeingia hatua ya robo fainali ambapo sasa mechi zinachezwa
kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam.
Uamuzi wa
kuhamisha mechi hizo kutoka viwanja vya Karume na DUCE ni kuziwezesha zote
kuoneshwa moja kwa moja (live) na Azam Tv.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunaomba radhi kwa washabiki ambao watakuwa
wameathirika kutokana na uamuzi huo.
USAJILI
DIRISHA DOGO KUFUNGWA DESEMBA 15
Wakati
dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 15 mwaka huu, Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) tunazikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia
muda uliowekwa.
Pia
tunakumbusha kuwa kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi
nafasi ya kusajili mchezaji mpya. Kama klabu ilisaji wachezaji 30 maana yake ni
kuwa haina nafasi ya kuongeza wachezaji.
Kwa upande
wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa kuanzia msimu ujao
2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa.
Kuhusu
usajili wa wachezaji kutoka nje mpaka sasa hakuna hata klabu moja imeshaingia
kwenye TMS kuomba uhamisho. Itakapofika Desemba 15, system ya TMS itafunga.
RAMBIRAMBI
MSIMBA WA ANDREW KILOYI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha
mwamuzi wa zamani wa FIFA, Andrew Kiloyi kilichotokea mjini Iringa.
Kwa mujibu
wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa, Ramadhan
Mahano, Kiloyi alifariki dunia juzi (Novemba 24 mwaka huu) kutoka na ugonjwa wa
fangasi ya ubongo, na marehemu amesafirishwa kwenda kwao Kigoma ambapo
atazikwa.
Kiloyi
alizaliwa Mei 5, 1968. Alijiunga na uamuzi wa mpira wa miguu mwaka 1988 ambapo
alipata beji ya FIFA mwaka 2001 akiwa mwamuzi msaidizi. Alistaafu uamuzi mwaka
2009, na hadi anafariki akiwa mjumbe wa Kamati ya Waamuzi ya Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Iringa (IREFA).
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pole kwa familia ya marehemu, IREFA,
ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwataka kuwa na moyo wa
subira na uvumilivu katika kipindi hicho cha majonzi. Mungu aiweka mahali pema
roho ya marehemu Kiloyi.
No comments:
Post a Comment