Picha haihusiani na habari hii ila ni baadhi ya ajali zinazopoteza uhai wa watanzania wenzetu barabarani. |
AJALI zimeendelea kunyofoa roho xa wenzetu baada ya watu 12 kuripotiwa kufariki katika ajali ya basi lililotokea Korogwe Tanga, huku wengine wakiachwa hoi na majeraha ya ajali hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa hivi punde na Radio One, abiri hao walikumbwa na mkasa huo baada ya basi walililowa wakisafiria la Burudan kutoka Korogwe kwenda Dar kuacha njia yna kupinduka katika kijiji cha Taula, wilayani Handeni.
Taarifa zaidi zitawajia kujua kinachoendelea katika ajali hiyo ambayo ni mfufulizo wa matukio yanayopoteza uhai wa watanzania wenzetu na wengine kuachwa wakina ulemavu wa kudumu.
No comments:
Post a Comment