STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 12, 2013

Hii ndiyo taarifa rasmi ya ajali ya basi la Burudan



WATU 12 wamekufa papo hapo huku wengine 71 kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali basi la abiria la Kampuni ya Burdan kupinduka katika kona ya Kwaluguru kata ya Kabuku wilayani Handeni Mkoani Tanga leo asubuhi.

Basi hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Korogwe Dar es Salaam lilipata ajali majira ya ya asubuhi kutokana na mwendo kasi uliopelekea dereva kushindwa kumudu gari hilo na kuacha njia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,Costantine Massawe amethibitishwa kutokea kwa ajali hiyo,na kusema majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Wilaya Magunga kwa ajili ya matibabu.

Kamanda Massawe alitaja namba za gari hilo kuwa ni T.610 ATR aina ya Nisani lilikuwa likitokea Korogwe likielekea Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Luta Mpenda ambaye alipoteza maisha papo hapo.

Mwendo kasi unatajwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali ambayo majeruhi imeitaka serikali kusimami kikamilifu na kuchukua hatua kwa madereva wanao kikuka sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akaiomba serikali kuboresha huduma za afya kwenye hosptali hiyo ili kuondokana na changamoto iliyojitokeza ya ukosefu wa damu.

Majeruhi wengine 19 wamepelekwa katika kospitali ya KCMC Moshi na Moi Dar es Salaam kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

No comments:

Post a Comment