BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika desemba 31
siku ya kufunga mwaka katika ukumbi wa msasani klabu ambapo atatupiana
makonde na Mohamed Kashinde katika mpambano wa raundi sita siku hiyo
akizungumza na waandishi wa habari kocha
wa kimatafa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa king class kesha ingia kambini kwa ajili ya mpambano uho wa
kufunga mwaka kwani ndio itakuwa mpambano wa mwisho kabisa kwa mwaka
uhu
bondia king class mawe yupo fiti na ana
juhudi binafsi ya kujituma mazoezini ndio siri ya mafanikio aliyo nayo
mpaka sasa na kuweza kuwachachafya mabondia mbalimbali nchini ikumbukwe
kuwa class ni bondia chipkizi lakina amesha wachakaza mabondia wakongwe
kama Amosi Mwamakula,Simba Watunduru na Said Mundi wa Tanga na Patrick
Kavako wa Morogoro ambao wote hawo kawachakaza kwa vipindi tofauti hivyo
Kashinde ajiandaee sana
kwa ajili ya kupambana na King Class Mawe
Katika mchezo huo kutakuwa na michezo
mingine ambapo bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi
Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine
ni kati ya Fransic Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga
kutoka Kenya
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria
zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
No comments:
Post a Comment