Mzee Nelson Mandela enzi za ujana wake |
THE UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika
ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote
na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela
kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu
sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".

Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za
maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.
Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Mwisho.

Imetolewa
na;
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.
No comments:
Post a Comment