Ronadinho (kulia) akidhibitiwa a beki wa Raja Casablanca |
RONALDINHO alivamiwa na mashabiki ambao walimvua viatu na kumuomba jezi yake baada ya wenyeji Raja Casablanca kuishangaza timu ya Atletico Mineiro ya mwanasoka bora huyo wa dunia wa zamani kwa kuifunga magoli 3-1 juzi.
Raja Casablanca walifunga mara mbili katika dakika 10 za mwisho katika mechi hiyo ya nusu fainali na kutinga fainali itakakokumbana na Bayern Munich Jumamosi.
Raja, ambao walifuzu kama mabingwa wa taifa mwenyeji Morocco, walipata goli la kuongoza la mapema kipindi cha pili wakati Mouhssine Lajour alipobaki peke yaje na kufunga kwa shuti la chini.
Lakini nyota wa zamani wa Barcelona na AC Milan, Ronaldinho alifunga kwa 'fri-kiki' ya hatari iliyokwenda wavuni baada ya kugonga nguzo ya lango na kuwasawazishia mabingwa hao Ligi ya Klabu Bingwa Amerika ya Kusini.
Raja walirejesha uongozi wao katika dakika ya 83 kwa penalti ya utata wakati Rever alipoambiwa kwamba amemuangusha Lajour, ingawa picha za marudio za televisheni zilionyesha hakuguswa.
Mohaine Moutaouali alifunga penalti hiyo ya utata katioka dakika ya 83 na Vivien Mabide akakamilisha ushindi katika dakika ya nne ya majeruhi kwa goli la shambulizi la kustukiza.
Mwisho wa mechi hiyo mashabiki wa Raja walimzunguka Ronaldinho kumuomba jezi yake na wakamvua viatu vyake.
Raja sasa watacheza dhidi ya mabinwa wa Ulaya Bayern Munich katika fainali kesho mjini Marrakech.
Itakuwa ni mara ya pili tu tangu 2005 michuano hiyo ianze kuchezwa katika mfumo wa sasa kwamba fainali haihusishi timu za Amerika Kusini na Ulaya.
No comments:
Post a Comment