Kara Mbodji akishangilia bao la kusawazisha la Senegal dhidi ya Afrika Kusini |
Asamoah akishangilia bao pekee la Ghana dhidi ya Algeria |
Ubabe mtupu kati ya Algeria na Ghana |
Bafana Bafana walishindwa kulinda bao lao dhidi ya Senegal katika mechi iliyochezwa usiku wa jana na kuambulia pointi moja ikiwaacha wakiwa mkiani mwa msimamo wa kundi hilo la 'kifo'.
Afrika Kusini walioanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 3-1 na Algeria, walitangulia kupata bao dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Oupa Manyisa kabla ya Senegal walioilaza Ghana kwenye mchezo wao wa kwanza kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Kara Mbodji.
Sare hiyo imeiweka Senegal kileleni mwa kundi hilo wakiwa na pointi nne wakifuatiwa na Algeria ambayo ilicharazwa bao 1-0 na Ghana iliyopo nafasi ya tatu kwa bao la dakika za jioni lililowekwa kimiani na nahodha wa Black Stars, Asamoah Gyan.
Kivumbi cha michuano hiyo kuhitimisha raundi ya pili kitaendelea leo kwa michezo ya kundi D ambapo Mali watavaana na Ivory Coast kabla ya Cameroon kujiuliza kwa Guinea. Timu zote nne katika mechi zao za awali waliambulia sare ya 1-1 na hivyo kulingana kwa kila kitu katika kundi hilo.
No comments:
Post a Comment