Abdi Kassim |
KIUNGO
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' anatarajiwa
kuanza rasmi kibarua chake nchini Malaysia leo( Jumanne) atakashukla
dimbani na timu yake ya UiTM kuumana na PBDKT T-Team katika mechi ya
Kombe la FA.
Pambano hilo linaloashiria kuanza upya kwa msimu wa Ligi nchini Malaysia litachezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa UiTM wa Mini UITM, uliopo mji wa Shah Alam.
Kwa mujibu wa Babi mechi hiyo ndiyo ya kwanza ya mashindano kwake kabla ya Ijumaa kuanza kipute cha Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa kuumana ugenini na klabu ya Kuala Lumpur SPA.
"Kesho (leo) tunatarajia kushuka dimbani kwenye mechi ya FA dhidi ya T-Team inayocheza Super League, kabla ya Ijumaa kuanza kipute cha Ligi kwa kuvaana na Kuala Lumpur SPA ugenini na baadaye kurejea nyumbani kucheza na Johor," alisema.
Babi alisema yupo fiti kwa ajili ya msimu huo anaoucheza kwa mara ya kwanza nchini humo akiwa mmoja wa wachezaji tegemeo hasa baada ya kufanya mambo kwenye mechi kadhaa za kirafiki za kujipima nguvu.
Mchezaji huyo alitua katika timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMKM iliyomsajili na kuichezea klwa muda mfupi akitokea Azam aliomaliza nao mkataba na kuichezea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

No comments:
Post a Comment