BASI Likiwa limeanguka na maiti bado zilikuwa hazijatolewa chini huku dimbwi la damu likionekana |
Na Abdulaziz Video, Lindi
WATU 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi.
Ajali hiyo iliyotokea mchana leo baada ya basi hilo kupishana na lori na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti wote wamefikishwa hospitali.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, George Mwakajinga ambae alikuwepo katika eneo la ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na kutingwa na harakati za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo.
AJALI NYINGINE zachukua uhai wa watu 3 Same;
9 Manyara; 9 Lindi; 13 Singida
MANYARA: Woinde
Shizza kutoka Arusha ameandika kwenye blogu yake kuwa watu 9 wamefariki
dunia hivi punde huku mmoja akinurusika baada ya kufukiwa na kifusi
wilayani Karatu, Mkoa Manyara wakati wakichimba mchanga katika eneo
ambalo lilikuwa limezuiwa na Serikali, lakini watu hao wameanza tena
kuchimba hivi karibuni.
KILIMANJARO: Katika
taarifa ya habari ya Radio Sauti ya Injili, Moshi jioni hii,
imeripotiwa kuwa watu watatu wamepoteza uhai huku wengine 30 wakiachwa
na majeraha mbalimbali wakati basi la kampuni ya Hood lenye namba
T.497AHD walilokuwa wamepakia kutokea Iringa kuelekea Arusha, lilipopata
ajali majira ya saa 11 jioni kwa kuacha njia na kuanguka katika eneo la
Nkwini, huko Makanya-Hedaru katika barabara ya Same-Mombo wilayani Same
mkoani Kilimanjaro.
Majeruhi wawili hali zao zimeelezwa
kuwa mbaya hivyo kuwahishwa katika hospital ya rufaa ya KCMC. Majeruhi
wengine wawili walitibiwa katika kituo cha afya cha Hedaru wakati miili
ya marehemu waliotajwa na Robert Boaz (Kamanda wa
Polisi
mkoani Kilimanjaro), kuwa ni Stephano Kasimba, Fadhili Kasimba na Aziza
Mdee, imehifadhiwa katika hospitali ya Same ambako majeruhi wengine 25
wanaendelea na matibabu.
Walionurusika kifo wamesema basi hilo
halikuwa katika mwendo ila dereva wake aliyetajwa kwa jina la Baraka
Juma, alionekana kuwa mchovu na huenda ajali hiyo imetokana na usingizi
uliomkumba dereva huyo ambaye ametoroka baada ya ajali hiyo kutokea.
LINDI: Taarifa
ya TBC Taifa iliyosomwa saa mbili usiku huu inasema kuwa, watu 9
wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa
vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake
kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka chana wa leo katika
kijiji cha Mambulu huko katika manispaa ya Lindi, wakati likipishana na
lori kabla ya kupoteza mwelekezo na kupinduka wakati mvua kali
ikinyesha.
SINGIDA: Imeripotiwa
katika taarifa ya TBC saa saba mchana na mbili usiku uu kuwa jumla ya
abiria 13 wakiwemo watatu wa familia moja, wamefariki dunia mkoani
Singida leo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK,
kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB.
Ajali hiyo ya mbaya iliyoacha miili
ikiwa haitamaniki, imetokea leo mwendo wa saa moja asubuhi katika
barabara kuu ya Singida-Dodoma kwenye eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya
Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,
SACP, Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea
Itigi kuelekea Singida Mjini huku lori lililokuwa likitokea Mwanza
kupitia Singida kuelekea Dar es Salaam, wakati likipishana na Noah hiyo,
lilihama upande wake na kuifuata Noah upande wa kushoto na kuigonga na
kuiburuza: “...baadhi ya watu wanadai kuwa huenda dereva wa lori
alisinzia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata Noah.
Uchuguzi utakapokamilika tutatoa taarifa hiyo,” amesema.
Hadi sasa miili ya marehemu
iliyokwishakutambuliwa na ndugu zao ni pamoja na Omari Shaaban (44) na
mkewe Salma Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi
Mjini. Haji Mohammed (29) (Msisi), Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),
Salehe Hamisi (28) (Sajanranda), Samir Shaban (20) (Puma), Mwaleki
Nkuwi (35) (Ikungi), Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga
(Sajaranda).
Miili ambayo haijatambuliwa imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, mjini Singida.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa
mjini Singida, Dk. Banuba Deogratius amekiri kupokea miili ya watu 13,
wawili kati yao wakiwa ni watoto.
Katika ajali hiyo, abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo.
Source: http://www.wavuti.com
No comments:
Post a Comment