Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi, japo baadhi ya wachezaji hawakwenda Afrika Kusini |
Wenyeji Afrika Kusini wanaotarajiwa kuwavaa Mali jioni hii |
MAJIRANI wa Tanzania na wawakilishi wengine wa ukanda wa CECAFA, Burundi jana ilianza michuano ya CHAN 2014 kwa kulazimishwa suluhu na Gabon katika mechi ya kundi D.
Suluhu imeifanya Burundi kuvuna pointi moja na kukamata nafasi ya pili nyuma ya DR Congo ambayo mapema jana iliitambia Mauritania kwa kuilaza bao 1-0 kwa mkwaju wa penati ambayo ilimponza beki wa Mauritania kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea muda mchache ujao kwa wenyeji Afrika Kusini kuvaana na Mali huku timu zote zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za kwanza dhidi Nigeria na Msumbiji ambazo zitaumana baadaye usiku huku zote zikiwa majeruhi.
Afrika Kusini iliifumua Msumbiji kwa mabao 3-1 wakati Nigeria ilijikwaa kwa majirani zao Mali kwa mabao 2-1, hivyo kufanya mechi za leo kutoa taswira ya timu zipi zitakazokuwa zikijitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele au kuaga mapema michuano hiyo.
Nigeria ambayo ni Mabingwa wa Afrika (AFCON) huenda leo isikubali kufanywa asusa tena na Msumbiji ambayo itakuwa ikisaka pointi za kuwafanya waendelee kujipa matumaini ya kuvuka salama kwenye kudni la ambalo linaoonekana lina ushindani kama lilivyo kundi C lenye timu za Libya, Ghana, Ethiopia na Jamhuri ya Kongo.
No comments:
Post a Comment