MABINGWA wa Mtani Jembe na washindi wa pili wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, Simba inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumamosi kuumana na Mtibwa Sugar.
Mchezo huo wa kirafiki utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa utakuwa wa mwisho kwa Simba, kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, alisema wameamua kupata mechi moja katika uwanja wa taifa kabla ya kuanza kwa ligi.
Matola alisema sababu kuu ya kuamua kucheza mchezo huo ni moja ya sehemu yao ya kuipa timu yao mazoezi katika uwanja wa Taifa, ambao itachezea mechi zake za nyumbani.
Alisema wameamua kucheza mechi na timu ya Mtibwa,
kwa sababu wanaitambua bora wake, hivyo wakicheza nayo inawapa maandalizi mazuri.
Matola alisema kuwa mchezo huo utafanyika majira ya saa 10.jioni, ikiwa ni moja ya sehemu ya kocha wao Zdravko Lugarusic, kutaka timu ngumu, ya kucheza na Simba.
"Haya ni maamuzi ya kocha mkuu Logarusic, anataka kuichezesha timu yake na timu ngumu, ambayo itaipa mazoezi mazuri timu yake, kabla ya kuanza kwaa ligi kuu" alisema Matola.
Simba iliyorejea juzi jijini Dar es Salaam, ikirtokea Zanzibar katika michuano ya Mapinduzi, ambapo ilifika hatua ya fainali na kupataushindi wa pili wa michuano hiyo.
SHAFII
No comments:
Post a Comment