THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:
255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE
HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA UMMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko
(Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo
mjini Zanzibar ambako leo ameungana na
Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12,
mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na
mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa
kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza
katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi
hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza
kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Rais Shein alitangaza mapumziko hayo
wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika
kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Mwisho.
Imetolewa na;
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
es
Salaam.
12
January, 2014
No comments:
Post a Comment