Alikuwa waziri mkuu wa Israel mwaka 2001.
Amekuwa mahututi tangu
mwaka 2006 kufuatia mfululizo wa matatizo ya kiharusi.
Ariel Sharon
alikuwa askari wa vita na baadae kuwa kiongozi wa nchi.
Alipokuwa mwanajeshi, alijulikana kwa ushujaa wake katika uwanja wa
mapambano kwa miongo kadhaa kufuatia kuundwa kwa taifa la Israel,
akijulikana hasa wakati wa vita vya jom kippur vya mwaka 1973. Katika
mbinu za hali ya juu alizozionyesha, aliwaongoza wanajeshi wa Israel
kuvuka mfereji wa suez, na kulikabili jeshi la misri.
Pia alijulikana na wengi kwa kuwa jabari na mbabe. Mwaka 1982,
aliongoza uvamizi wa Lebanon ambao ulipelekea mauaji yaliyofanywa na
wanamgambo wa Lebanon kwa mamia ya wapalestina katika kambi za wakimbizi
za sabra na shatilla huko Beirut.
Kama mwanasiasa, Ariel Sharon pia alikuwa na utatanishi. Akiwa
waziri, alihamasisha kuundwa kwa makazi ya walowezi wa kiyahudi kote
katika maeneo ya wapalestina.
Serikali yake ilizikandamiza vurugu katika muda wa miaka michache,
na kuanza kazi ya kuweka vizuizi vya usalama ambavyo hivi sasa
vinawatenga waisraeli na wapalestina.
Mwaka 2006, bwana Sharon alipata mfululizo wa matatizo ya kiharusi
na kuingia katika hali ya kupoteza fahamu. Nafasi yake ya waziri mkuu
ilichukuliwa na Ehud Olmert.Chanzo:VOASWAHILI.COM
No comments:
Post a Comment