Bobby Williamson |
Adel Amrouche |
Na Sanula Athanas, Zanzibar
MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga ameweka wazi kuwa pamoja na kupokea majina ya makocha 60 walioomba kazi ya kuifundisha timu hiyo, ni makocha wawili tu ambapo Yanga wameona wanauwezo wa kuifundisha timu hiyo.
Akizungumza mjini Zanzibar juzi usiku, Sanga alisema Kocha wa Gor Mahia, Bobby Williams raia wa Scotland na Kocha wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars), Mbelgiji Adel Amrouche, ndiyo makocha pekee wenye sifa za kuinoa timu yao inayokabiliwa na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika mapema mwezi ujao.
Sanga, aliyekuwa kisiwani hapa tangu juzi kwa ajili ya kuiomba radhi serikali ya Zanzibar kwa kutoleta timu yao kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi, alisema baada ya kufanya mchujo wa majina zaidi ya 60 waliyokuwa nayo makocha hao ndio wawili ndiyo wamekidhi vigezo vinavyotakiwa na klabu hiyo ya Jangwani.
“Unajua yanazungumzwa mengi kuhusu kocha wetu ajaye, lakini ukweli ni kwamba mpaka sasa hatujapata kocha mkuu na timu itaendelea kuwa chini ya Mkwasa (Boniface) hadi pale tutakapopata,” alisema kiongozi huyo.
“Tulipata zaidi ya maombi ya makocha 60, wanaotufaa ni Bobby na kocha wa Harambee Stars (Amrouche). Tumefanya mazungumzo nao lakini kuna masharti magumu yanayotuchelewesha kwa sababu wana mikataba na timu zao,” aliongeza Sanga.
Alisema kuwa bado wapo kwenye mazungumzo kuona ni kwa namna gani wanaweza kumpata kocha mmoja wapo kati ya hao kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kocha aliyetimuliwa, Ernest Brandts raia wa Uholanzi.
Kocha huyo alitimuliwa siku mbili baada ya kufungwa na Simba magoli 3-1 kwenye mchezo maalum wa kirafiki wa 'Nani Mtani Jembe' uliochezwa Desemba 21 mwaka jana.
Kikosi cha Yanga kwa sisi kipo chini ya Kocha Charles Mkwasa ambaye amchukuliwa pamojana Juma Pondamali kuchukua nafasi za Fred Felix 'Minziro' na Mkenya Razaq siwa ambao pia walitupiwa virago pamoja na Brandts.
Yanga ipo nchini Uturuki ilipokwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu pamoja na ligi ya klabu bingwa Afrika.NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment