MANCHESTER United ambayo inauguza maumivu wa kung'olewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi (Capital One) usiku wa kuamkia leo, imekubali kulipa ada ya pauni milioni 37 ambayo ni rekodi kwa klabu ili
kumnasa Juan Mata kutoka Chelsea.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho ameidhinisha dili hilo baada ya mazungumzo na
maofisa wa klabu na sasa Mata anatarajiwa kufanyia vipimo leo na kusaini mkataba wa miaka minne na nusu.
Mtendaji
mkuu wa Manchester United amekubali kuvunja rekodi ya klabu ya usajili
kwa ajili ya Mata ili kuokoa msimu unaokwenda kombo kwao.
Vipigo
saba katika Ligi Kuu ya England vimeiacha United ikiwa nyuma kwa pointi
6 kutoka nafasi ya nne kwanye msimamo wa Ligi ambayo ingewawezesha
kushiriki Champions League msimu ujao – lakini kuongezeka kwa Mata
kunatarajiwa kuleta uhai mkubwa.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi jana walitolewa na Sunderland kwenye michuano ya Kombe la Ligi kwa kufungwa mikwaju ya penati 2-1 baada ya kumaliza dakika 120 wakishinda 2-1 nyumbani na kulingana na Sunderland waliowafungwa kwao idadi kama hiyo.
Kitu kilichosikitisha ni kwamba katika penati tano walizopiga Man Utd walipata moja tu huku tatu zikishindwa kuingia kimiani.
No comments:
Post a Comment