Na Daud Julian
Akizungumza na mtandao huu, katibu mkuu wa chama hicho, Hemed
Mumba alisema maandalizi kwa ajili ya kozi hiyo itakayochukua siku kumi
yanakwenda vizuri na kwamba tayari baadhi ya makocha wameshajiandikisha.
Mumba alisema lengo
la kozi hiyo ni kuwaendeleza makocha wa mpira wa miguu mkoani Morogoro na mikoa
mingine ili kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua kubwa.
Alisema ada ya
ushiriki katika kozi hiyo ni Sh.60,000 na mwisho wa kulipa ada hiyo ni Februari
16.
Katibu huyo alisema
ada inatakiwa kulipwa kwa mweka hazina wa chama au katibu mkuu katka ofisi za
chama hicho zilizopo ndani ya ofisi za chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA)
na mshiriki ahakikishe anapewa risiti.
“Maandalizi kwa ajili
ya kozi hii yanakwenda vizuri na makocha wameanza kujitokeza lakini pia milango
ipo wazi hata kwa makocha walio nje ya Morogoro kuja kuchukua mafunzo haya”,
alisema.
Kozi hiyo ni ya
kwanza kutolewa na chama hicho chini ya uongozi mpya ulioingia madarakani hivi
karibuni chini ya mwenyekiti wake, John Simkoko.
No comments:
Post a Comment