Pamoja na Mata kuonyesha kiwango, Man Utd wamelala muda mfupi uliopita 2-1 |
Kevin Miralla akiifungia Everton bao la ushindi dhidi ya Aston Villa |
Shane Long akiifungia Hull City bao la kuongoza dhidi ya Spurs |
UGONJWA unaoisumbua Manchester United msimu huu katika Ligi Kuu ya England bado haujapata tiba, bali ulikuwa umepoa baada ya jioni hii kukandikwa ugenini mabao 2-1 na Stoke City, huku Everton kushinda nyumbani magoli 2-1 dhidi ya Aston Villa.
Mashetani Wekundu hao ambao walizinduka mapema wiki hii kwa kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Cardiff City, ilishindwa kuendeleza makamuzi yake kwa kulala katika mchezo na kuzidi kuwakosesha raha mashabiki wa klabu hiyo.
Vijana hao wa David Moyes, walienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 baada ya wenyeji kupata bao la dakika ya 38 kupitia kwa Charlie Adam kabla ya kulisawazisha dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili kupitia kwa Robin van Persie.
Hata hivyo Charlie Adam aliipigilia msumari mwingine katika 'jeneza' na Man United katika dakika ya 52.
Katika mechi nyingine, Everton ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa, huku Southampton ikiwa ugenini ilipata ushindi wa magoli 3-0 dhidi y Fulham.
Tottenham Hotspur walishindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Hull City na Cardiff City kutamba nyumbani kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Norwich City.
No comments:
Post a Comment