HIVI karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu yetu ya mpira, uongozi na baadhi ya wanachama.
Ni haki na ni kwa nia njema tu ya wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi, Ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo mema na mabaya.
Ushindi au mwenendo mzuri wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, Wachezaji, Walimu, Viongozi, Wanachama na wapenzi kwa ujumla.
Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha technical bench yote na kutoa adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi kilichopita.
Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli haupo ama kwa faida zao binafsi, au kwa kutumiwa na watu wa nje kutuvuruga na kuondoa amani klabuni.
Habari zilizoandikwa na moja ya gazeti maarufu za kusema Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa Ndugu Seif Ahmed kuwa si mwanachama halali wa YANGA, eti anahujumu timu na yupo kwa maslahi yake binafsi ni za uzushi na hazina ukweli wowote.
Habari hizi zimelenga kuwakatisha tamaa na kuwavunja moyo viongozi wetu ambao wapo mstari wa mbele katika kujenga YANGA. Watu hawa ni hatari sana na hawaitakii merna YANGA na wanafanya hujuma hizi kwa malengo ya kuwapandikiza viongozi vibaraka wa kuidhoofisha timu yetu na kutimiza malengo yao binafsi.
Uongozi ungependa kutoa tahadhari kwa wanachama kuwa hizo ni mbinu chafu ambazo zimelenga kutudhoofisha na kutusambaratisha.
Wachochezi hawa kwa nyakati tofauti wamekuwa pia wakutuma ujumbe wa simu wenye vitisho na matusi kwa kiongozi huyu na baadhi ya viongozi wenzake.
Tunatoa onyo kwa wale wote wanaotuma ujumbe wa simu wenye uchochezi na matusi, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao mara watakapofanya hivyo tena.
Tunawaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia sana kuzorotesha michezo nchini.
Uongozi unawaomba Wana Yanga kutulia na kutoa ushirikiano katika kupambana na njama hizi ambazo zinawe a kutudhoofisha tusipokuwa waangalifu ili tushindwe kufikia malengo yetu.
YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
Yusuf Manji
Mwenyekiti wa Yanga
Credit:Young Africans Official's Club
No comments:
Post a Comment