STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 27, 2014

Real Madrid 'yaua', Chelsea angalau Ligi ya Mabingwa Ulaya

Didier Drogba akionyesha manjonjo yaike mbele ya John Terry wa Chelsea jana ambapo timu zao zilitoka sare ya 1-1

Bale na Ronaldo wakipongezana wakati wakiiua Schalke 04 nyumbani kwao Ujerumani jan
REAL Madrid ikiwa katika kiwango cha hali ya juu msimu huu imevunja mwiko wa kushindwa kushinda kwenye ardhi ya Ujerumani baada ya usiku wa kuamkia leo kuifumua Schalke 04 kwa mabao 6-1 na kunusu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Chelsea ya England ikibanwa ugenini na Galatasaray na kutoka sare ya 1-1 nchini Uturuki.
Mabao ya Karim Benzema katika dakika ya 13, kisha Gareth Bale kwenye dakika ya 21 yaliifanya Madrid kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 kabla ya kurudi kipindi cha pili wakiwa moto zaidi na kuongeza mabao mengine manne.
Cristiano Ronaldo alifunga bao dakika ya 52 kabla ya Benzema kurudi tena nyavuni dakika mbili baadaye na Bale kuongeza jingine dakika ya 69 na Ronaldo kumalizi udhia dakika ya 89.
Wenyeji waliambulia bao lao la kufutia machozi dakika moja ya nyongeza (90+1) kupitia kwa mdachi,  Klaas-Jan
Huntelaar na kuifanya Schalke 04 kuwa na kibarua kigumu cha kuweza kupata ushindi wa mabao 5-0 ugenini ili kuing'oa vinara hao wa Ligi ya Hispania.
Katika pambano jingine la kuhitimisha mechi za mkono wa kwanza za 16 Bora Chelsea ikiwa ugenini ilitangulia kuwafunga wenyeji kwa bao la Fernando Torres dakika ya 9 tu ya mchezo na kutoa matumaini huenda vinara hao wa Ligi ya England wangeibuka na ushindi ugenini na kuifuta machozi nchi yao ambayo imeshuhudia timu zake nyingine tatu zikifungwa katika mechi zake za mkondo huo.
Hata hivyo Chelsea walishindwa kulinda bao hilo kwani wenyeji Galatasaray walikuja kuchomoa bao dakika ya 65 kupitia kwa Mcameroon,  AurĂ©lien Bayard Chedjou  aliyemalizia mpira wa kona uliochongwa na Mdachi Wesley Sneijder na mabeki wa Chelsea wakazembea kumkaba na kumfunga kirahisi kipa wao Petr Cech .

No comments:

Post a Comment