Gari la Hood likiwa limepinduka na majeruhi wakipigania uhai wao |
Abiria wakiwa hawaamini kama wamenusurika kifo |
AJALI zimeendelea kutikisa Tanzania, baada ya Basi
la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili
T.488 AXV aina ya Scania kupata ajali mbaya leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na abiria wengine karibu 20 kujeruhiwa.
Ajali
hiyo imetokea majira ya saa tatu katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya
mbele.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la
Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda
Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili
Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani
Kilimanjaro, KCMC.
Kamanda
Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8
wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa
mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi.
No comments:
Post a Comment